OUR VISION, MISSION, OBJECTIVES, AND MEMBERS

MAONO:VISION

Kuwa na vijana walioelimika kiroho,kimwili na kuwajibika kikamilifu kwa jamii na Mungu.

UTUME: MISSION

Kuendeleza kazi ya kuboresha maisha ya vijana kwa kuwaunganisha vijana,kuwapa elimu ya Neno la Mungu na stadi za maisha,kuwafunza maadili mema,kuwasaidia kuwa na bidii katika kazi za uzalishaji ,na kujiepusha na mambo yanayohatarisha maisha yao.

MALENGO: OBJECTIVES

-Vijana wasichana na wavulana kwa pamoja kushirikiana katika kuyaongoza maisha yao katika mambo mbalimbali ya kiroho,kwa kuwa na uongozi wao na ulezi wa kanisa.

-Kutambua fursa zilizopo na zinazotuzunguka na kuzitumia kwa pamoja katika ujenzi wa kanisa na maisha kwa ujumla

-Kuibua, kuendeleza na kutumia vipaji katika kuitangaza injili kwa watu wote.

-Wakiongozwa na Roho Mtakatifu kujenga tabia zao,Nchi yao,Kanisa lao kwa kujiunga katika mawazo na matendo ya kumpendeza Mungu sawasawa na Neno lake.

-Kushirikiana na vijana wengine ndani na nje ya nchi

-Kuwa na vijana waliompokea Yesu Kristo kuwa Bwana wa maisha yao.

-Kujitagemea katika mahitaji ya kimwili ikiwa njia ya kufanya kazi kwa bidii na maarifa.

-Kukuza ujuzi wao kiroho na kiakili kwa njia ya kujifunza Neno la Mungu na maarifa mbalimbali ya kimaendeleo na kiuchumi.


WALENGWA: MEMBERS

VIJANA WOTE WALIO NDANI YA KANISA NA NJE YA KANISAWENYE UMRI KUANZIA MIAKA 15-45

Sunday, December 29, 2013

Glory choir!


No comments:

Post a Comment